Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya, imefikia watu 15 na huku wengine ambao idadi yao haijajulikana wakijeruhiwa baada ya kusombwa na mafuriko maeneo mbalimbali nchini humo.
Taarifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imedai kuwa, maelfu ya watu wameachwa bila makao huku ikisema huenda hasara kubwa ikapatikana kutokana na ukubwa wa mvua hizo zinazoendelea kunyesha.
Aidha, inaarifiwa kuwa pia mgogoro wa kibinadamu huenda ukashuhudiwa kutokana na athari za mafuriko yanayoshuhudiwa nchini Kenya hasa maeneo ya pwani, Kaskazini Mashariki, bonde la ufa na magharibi mwa Taifa hilo.
ZMafuriko hayo, yameleta athari kubwa kufuatia zaidi ya familia 15,000 kuathiriwa, mifugo zaidi ya 1,000 kufariki na mazao ya mashamba kiasi cha heka 241 kuharibiwa huku Mbunge wa Nyandarua, Faith Gitau akisema pia shughuli za usafiri zimetatizika.