Mafuriko nchini Libya, yameua takriban watu 6,000 huku wengine wapatao 10,000 wakiwa wametoweka baada ya kusombwa hadi kwenye bahari ya Mediterranean au kufunikwa kwenye tope, serikali imesema Jumatano.

Shirika moja la Habari nchini humo, limesema wengi waliokoseshwa makao walikuwa wakiishi kwenye mji ulioharibiwa wa Derna, wakati maelfu wengine wakiwa ni kutoka maeneo mengine, ukiwemo mji wa Benghazi.

Wakati huo huo, shirika la Kimataifa la Uhamiaji limesema kwamba mafuriko hayo mashariki mwa Libya yamekosesha makazi zaidi ya watu 30,000 huku

Mabwawa mawili, yalivunja kingo juu ya mji wa Derna na kuongeza mafuriko yaliokuwa yamesababishwa na mvua kutokana na kimbunga Daniel ambapo idadi kamili ya vifo huenda isijulikane kutokana na ushindani wa serikali mbili, baadhi ya maafisa wakisema kwamba huenda ikawa mara mbili.

Serikali yasisitiza uzingatiaji mwongozo Takwimu za Sensa
Watanzania wanataka Umeme wa uhakika - Dkt. Biteko