Idadi ya watu waliokufa kutokana na Tetemeko la ardhi nchini Indonesia imeongezeka kufikia watu 268 wakati vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta manusura kutoka vifusi vya udongo.
Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo alitembelea eneo lililoathiriwa zaidi la kitongoji cha Cianjur, kusini mwa mji mkuu wa Jakarta, na akaahidi kuwalipa fidia wahanga wa janga hilo na kuwahimiza wakoaji kuongeza kasi ya kuwatafuta manusura.
Aidha, Widodo pia amezungumzia pia suala la kuyajenga upya majengo yaliyoporomoka akisema itasaidia kuwarahisishia watu hao kupata sehemu za kuishi kama moja ya msaada.
Tetemeko hilo la ukubwa wa 5.6 katika kipimo cha Ritcher, limewajeruhi zaidi ya watu 1,000, kuharibu miundombinu na kufukia watu chini ya vifusi vikubwa vya udongo.