Wahitimu 2,194 wa Elimu ya msingi, ambao waliofutiwa matokeo kutokana na udanganyifu wamepewa nafasi nyingine na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), kufanya mtihani wa marudio.
NECTA imesema, watahiniwa ambao shule zao zimefungiwa kuwa vituo vya mitihani, watafanya kwenye vituo vya jirani na shule zao na kwamba mtihani huo wa marudio utafanyika Desemba 21 na 22, 2022.
Desemba mosi, 2022 NECTA ilitangaza matokeo ya darasa la saba na kuwafutia matokeo yote ya Watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa 1,350,881 waliofanya mtihani, waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.
Hata hivyo, NECTA ilisema kitakwimu kuna uwepo wa kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka jana (2021).