Taharuki! Wafungwa wawili wametoroka katika gereza lililo na ulinzi wa juu nchini china, nchi ambayo wafungwa wake wanalindwa sana na ni vigumu kutoroka.
Wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela ina aminika kuwa bado hawajaenda mbali na maeneo ya gereza hilo.
Wang Lei mwenye umri wa miaka 33 na Zhang Guilin mwenye umri wa miaka 39 walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la utekaji na unyang’anyi wa mali mnamo mwaka 2017.
Zhang Guilin alijaribu kutoroka zaidi ya mara mbili baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha kabla ya kufanikiwa kutoroka, na anasifika kwa ukorofi na kuwajeruhi wafungwa wenzake.
Kwa mujibu wa chombo cha habari “Beijing Youth Daily” kimeripoti kuwa wafungwa hao walitoroka wakiwa wamevaa sare na vitambulisho vya polisi walivyo iba, lakini radio ya taifa imetoa taarifa kuwa njia walizo torokea bado hazija thibitishwa ila inasadikika walitumia dirisha kutoka.
Hii sio mara ya kwanza kwa wafungwa kutoroka kwani mwaka 2014 wafungwa watatu walitoroka kutoka katika gereza lenye ulinzi wa juu, baada ya kuwauwa polisi na kuvaa sare zao lakini walipatikana baada ya wiki moja.
Serikali imetangaza donge la Dola 14,558 kwa wananchi watakao saidia kuwakamata wafungwa hao.