Mwanamuziki maarufu nchini Uganda ambaye amekuwa ni mbunge, Bobi Wine ametanabahisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba kikundi cha watu wasiojulikana kilimtesa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mbunge huyo kutoka kambi ya upinzani, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka kwa kurirushia mawe gari la raisi lililokuwa kwenye msafara wa Rais Yoweri Museveni mwezi uliopita na kukamatwa August 13 mwaka huu.
Aidha, Jeshi nchini Uganda limekana tuhuma dhidi yake na kuita kuwa ni upuuzi, huku rais Museveni akisema taarifa hizo ni za kizushi.
“Walinipiga,walinipiga na kunipiga kwa buti zao, hawakubakisha sehemu katika mwili wangu ambayo haikuguswa kwa kipigo, hawakubakisha. Walipiga kila sehemu ya mwili wangu, hawana utu hata kidogo hawa watu”amesema Bobi Wine
Hata hivyo, Bobi Wine amesema kuwa walizivuta sehemu zake za siri na kuziminya kende zake huku wakiendelea kumpiga na kubinya vidole vyake kwa kitako cha bastola.
-
Video: DC Busega atangaza fursa 8 zakuchangamkia wilayani kwake
-
Uwekezaji kutoka China kuifikisha Tanzania uchumi wa kati
-
BREAKING: Rais Magufuli akizungumza na wananchi Ukerewe