Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC imesema raia wake 10 ambao ni Wanafunzi wamefariki kufuatia shambulizi la anga lililofanyika Katika chuo Kikuu cha Kimataifa kilichopo mji mkuu wa Sudan, Khartoum Jumapili Juni 4, 2023.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya DRC, kupitia kwa Waziri Christophe Lutundula ilisema katika taarifa yake kuwa, “imepokea kwa masikitiko makubwa” mauaji ya raia wake yaliyotokea katika Chuo hicho Kikuu cha Kimataifa cha Afrika.

Alisema, kuna dalili kwamba mashambulizi hayo ya anga yalifanywa na jeshi la anga kwenye eneo linalokaliwa na wakazi wasio na silaha, wakiwemo raia wa kigeni na kwamba katika shambulio hilo baadhi ya Wanafunzi pia walijeruhiwa vibaya.

Aidha, Waziri huyo alisema Serikali ya DRC bado inasubiri maafisa wa Sudan kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo, baada ya Khartoum kujikuta katika mapigano kati ya jeshi na kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces – RSF, tangu Aprili 15, 2023.

JKT Tanzania: Tuna imani kubwa na Malale Hamsini
Ligi Kuu, ASFC marufuku Uwanja wa Mkapa