Nchini Botswana mwanafunzi wa chuo kikuu analipwa kiasi cha Dola za Marekani 154 ambazo ni sawa na shilingi laki tatu na elfu sitini na sita za Tanzania kila mwezi ili aende shule

Pia raia wa Taifa hilo mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anaweza kutuma maombi ya kupatiwa ardhi na hupewa bure kabisa.

Botswana ni kati ya mataifa yenye usalama wa hali ya juu zaidi Afrika kiasi kwamba hata Rais wa nchi anaweza kutembea mwenyewe mitaani bila walinzi

Raia wote pia wanapata bure huduma za afya na matibabu.

Serikali ya Botswana pia inatoa ruzuku kwa wazee na wenye matatizo ya kiafya na mwaka 2017 Bunge la nchi hiyo lilipitisha sheria ya wanafunzi kupatiwa taulo za kike bure kwenye shule zote nchini humo

Hiyo ndiyo Botswana.

Mshambuliaji KMKM azitaja Simba, Young Africans
Azam FC kumng'oa Peter Banda Simba SC