Wakati idadi kubwa ya watu wakiisifia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kuwakumbuka wanyonge, baadhi ya wanaharakati wameikosoa bajeti hiyo kwa kutokumbuka kupunguza gharama ya pedi za wanawake.

Mkurugenzi wa Baraza la Usambazaji maji, Wilhelmina Malima amesema kuwa ingawa serikali imeondoa kodi kwenye bidhaa mbalimbali, imesahau eneo muhimu zaidi la afya ya akina mama na wasichana.

Alisema kuwa wapo wanafunzi wengi wa kike ambao wamekuwa wakiacha shule kutokana na kushidwa kujihifadhi kwa usafi na usalama wanapokuwa katika siku zao za mwezi, na kwamba baadhi yao kutokana na kushindwa kumudu gharama za pedi wamekuwa wakitumia vipande vya nguo ambavyo sio salama.

“Tunawezaje kulinda haki za wanawake na wasichana bila kukumbuka afya yao kama kipaumbele cha kwanza?” alihoji.

Aliongeza kuwa bidhaa hiyo ni muhimu kwa kina mama wakati wa kujifungua, lakini ameshangaa kuona hali hiyo haipewi nafasi kwenye bajeti husika.

Naye Mkugugezi wa program ya mtandao wa jinsia (TGNP), Lilian Liundi ameliambia gazeti la The Citizen kuwa Serikali imekuwa ikiahidi kutoa kipaumbele kwa afya ya wanawake na wasichana lakini haijaonesha jinsi ambavyo itasaidia upatikanaji wa pedi kwa gharama nafuu.

Gharama za bidhaa hiyo imekuwa changamoto zaidi hasa maeneo ya vijijini na kwa familia masikini ambazo watoto wengi wametajwa kutohudhuria shule pale wanapokuwa katika siku zao.

Bosi EWURA atumbuliwa
Majaliwa apokea taarifa uchunguzi wa Salfa, Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar