Wananchi wilayani Nzega mkoani Tabora wameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kwa kuboresha huduma ya mtandao wa 4G wilayani humo.
Diwani wa Kata ya Nzega Mjini Magharibi, Godfrey Malema, amewasilisha pongezi hizo kwa niaba ya wananchi wakati akizindua duka la kisasa la Airtel Money lililopo mjini hapo mwishoni mwa wiki.
“Sisi wakazi wa Wilaya ya Nzega tuna furaha kubwa na tunatoa pongezi kwa kampuni ya mawasiliano ya Airtelkwa kutuboreshea huduma za 4G ambapo kwa sasa zinapatikana katika wiliya yote hii yote. Huduma hii ambayoina teknolojia ya kisasa ni msaada mkubwa kwetu kwani inatupa uhuru wa kuwasiliana na ndugu, jamaa namarafiki bila kikwazo chochote” amesema Malema.
Naye Mkuu wa Polisi wilayani Nzega, Costantine Mbogambi, aliipongeza Airtel kwa kuwapeleka huduma zamawasiliano ya uhakika karibu na wananchi.
“Zamani mtu akipoteza laini yake ya simu lazima aende makao makuu ya mkoa ili iweze kurudishwa. Leonimekuja hapa nikiwa na tatizo kama hili na nimefanikiwa kuirejesha namba yangu kwa muda mfupi sana,”amesema Mbogambi
Baadhi ya maeneo yeney minara iliyounganishwa na mtandao wa 4G kuwa ni pamoja na Ziba,Kitongo, Nzega Sokoni, Ushirika na Nhonge.