Wanawake wametakiwa kuacha kujihusisha na tamaduni zinazoweza kuchangia ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama Saratani, kwa kuweka ugoro sehemu za siri kwa madai kuwa inaongeza hamu ya tendo la ndao.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Ubora wa Ubunifu wa Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania – TCCP, Edna Selestine wakati wa Warsha ya usambazaji wa Data na Tafiti zilizofanywa na wataalamu wa maswala ya Saratani ikwemo taasisi ya Agha Khan, lengo likiwa ni kutoa uwelewa apamoja na namna ya kujikinga na maradhi hayo.
Amesema, mradi huo unaotekelezwa kwa miaka 4 kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Agha Khan Serikali ya Tanzania na shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD) umegharimu takribani mil. 34.5 za kitanzania ambapo wamefanya katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na zaidi ya watoa huduma mia nne wamepewa elimu juu ya maswala ya saratani.
“Kumekuwa na changamoto ya kuweka tafiti mbalimbali ambazo zimefanyika kuhusiana na changamoto ya kuweka ugolo sehemu za siri lakini kwakweli kwa kanda ya ziwa changamoto hii bado ni kubwa kwahi yo tunaendelea kutoa elimu kwa wanawake na sio ugolo peke yake kunamambo mengi siku hizi,” aliongeza Dkt. Edna.
Naye Meneja wa ubuia na mawasiliano – TCCP, Dkt Sara Maongezi amewataka Vijana kujikita zaidi katika kufanya tafiti zinazoendana na muktadha wa Tanzania ili kuwezesha majibu ya tafiti hizo kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya kitanzania.