Wamiliki wa Migodi Kata ya Saza Wilayani Songwe, wametakiwa kutatua changamoto zinazowakabili waajiriwa wao ikiwa ni pamoja na kuwalipa stahiki zao kwa wakati na kuwapa mikataba yenye tija, ili kuepusha migogoro isiyo na tija.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Theopista Mallya Dwakati wa kikao chake na wachimbaji wadogo wa Madini na Wamiliki wa Migodi katika eneo hilo cha kusikiliza kero, changamoto na kupata ushauri kuhusiana na mambo ya ulinzi na usalama.

Amesema, “Wamiliki wa migodi mmekuwa chanzo cha migogoro ambayo inapelekea kutokea kwa uhalifu na ukatili katika eneo hili kutokana na kutokutenda haki kwa waajiriwa wenu, walipeni mishahara hawa vijana pia wapeni mikataba yenye tija na acheni kuwatisha pindi wanapodai mishahara yao, ili kuondoa migogoro katika eneo hili.”

Aidha, Kamanda Mallya pia alihitimisha kwa kuwataka viongozi wa eneo hilo kwa kila mmoja kwenye nafasi yake kuwajibika na kutenda haki, ili kupunguza migogoro huku akiwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kutoa taarifa za uhalifu na kushiriki katika ulinzi wa maeneo yao.

Ihefu FC kutangaza Kocha mpya
Kocha Mtibwa Sugar aifungia kazi Young Africans