Licha ya kuwepo kwa Wadau mbalimbali wa kupinga uharibifu wa mazingira na Rasilimali za maji, bado hali ya uchafunzi imekua kubwa ambapo wanawake wametakiwa kushiriki kikamilifu katika harakati Hizo.
Wakizungumza mjini Morogoro Kwenye semina ya siku mbili February 22 na 23, 2023 iliyoandaliwa na Shahidi wa Maji, wanaharakati wa kutetea na kupinga uharibifu wa rasilimali za maji wamesema wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele.
Akitoa mada katika mkutano huo, Mmoja wa wanaharakati hao Gemma Akilimali amesema wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa Maji, na washirikishwe ipasavyo kwani wao ndio watumiaji wakubwa na wanatambua umuhimu wake.
Kwa upande wake, Afisa miradi Shahidi wa Maji, John Emanuel amesema Lengo la semina hiyo ni kutoa Elimu Kwa jamii, kuhusu umuhimu wa utunzaji vyanzo vya maji pamoja na rasilimali zake.
Amesema, anatambua jitihada zinazofanywa na serikali katika uthibiti uharibifu wa mazingira, lakini taasisi hiyo inaendela kukumbusha jamii umuhimu wa jambo hilo na athari zake
Serikali nchini, imekuwa ikiisisitiza jamii kutunza vyanzo vya maji pamoja na rasilimali zake ili kuepukana na changamoto ya uhaba wa huduma hiyo yanayotajwa kuchangiwa na mabadiliko tabia nchi.