Wizara ya Afya nchini Kenya, imetoa tahadhari ya uwepo wa ugonjwa wa mlipuko usiojulikana ambao umetokea eneo la magharibi mwa Kaunti ya Kakamega na kusababisha vifo vya watu wanne.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Afya Kenya, Patrick Amoth amesema ugonjwa huo uligunduliwa katika shule za upili za Mukumu Girls na Butere Boys, huku watu 627 wakiwa wakikutwa na ugonjwa huo hadi kufikia Aprili 14, 2023 alisema katika taarifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Afya Kenya, Patrick Amoth. Picha ya Anadolu.
Amesema, “kwa bahati mbaya, tumepoteza wagonjwa 4 kwa ugonjwa huu. Sisi katika Wizara ya Afya tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao, na Wizara ya Afya inasema dalili za ugonjwa huo ni homa, maumivu ya tumbo, kutapika na kuhara.”
Hadi kufikia jana (Aprili 14, 2023), uchunguzi wa kina ulikuwa ukiendelea ili kubaini sababu halisi na takwimu zilizochambuliwa zinaonyesha kuwa ugonjwa huo ulianza Machi 15, 2023 na tayari Serikali imeziofunga shule hizio mbili.
Hata hivyo, Wizara imesema tayari imechukua sampuli kadhaa za maji, chakula na tishu za binadamu kutoka maeneo yaliyoathirika kwa uchunguzi wa awali wa kimaabara na uchunguzi uliofanywa umefichua dalili zinazofanana na zile zinazoonekana kwa wagonjwa wa enterotoxigenic E. koli na salmonella typhi.
Aidha, vipimo vya maabara vya homa za kuvuja damu kwa virusi, ikiwa ni pamoja na Ebola, Marburg, Leptospirosis na Crimean-Congo hemorrhagic fever, homa ya dengue, Homa ya Bonde la Ufa na virusi vya West Nile vimekuwa hasi pia vimechukuliwa ili kuweza kubaini ukweli.