Kikosi cha Simba SC kimeanza Kambi ya Maandalizi ya Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani zao wa Jadi Young Africans, watakaokutana nao Jumapili (April 16) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema wachezaji wote waliokuwa majeruhi wakiongozwa na Aishi Manula, Henock Inonga, Augustine Okra na Saido Kanoute wamerejea kikosini.

Amesema Kanoute hajaonekana kwa sababu benchi la ufundi liliamua kumpumzisha na si mgonjwa.

“Okra yeye alikuwa majeruhi muda mrefu, lakini alipona na ameshaanza mazoezi, hakwenda Mbarali kwa sababu hakuwa na utimamu wa mwili, lakini naye pia amerejea kambini,” amesema Ahmed.

“Kama utakumbuka katika mchezo wetu wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Ihefu, beki wetu Inonga aliumia, alipata kidonda, ambaye hajaonekana katika mchezo uliofuata, ametibiwa na amerejea mazoezini na wenzake, Manula.”

“Kuhusu kiungo mkabaji, Kanoute tatu ni mzima na aliachwa kwa sababu ya kupata mapumziko, pia aliumia bega, akafanyiwa vipimo ikaonekana madhara yake si makubwa, akapewa mapumziko, naye amerejea mazoezini.”

Simba SC inahitaji kupata ushindi katika mchezo huo wa Jumapili ili kurejesha matumaini ya mbio za ubingwa wakati Young Africans inataka kujiimarisha kwenye msimamo na hatimaye kutetea taji hilo wanalolishikilia kwa sasa.

Viongozi wafundwe maadili, uzalendo: Nahodha
Tanzania mwenyeji wa ngumi Afrika