Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda ametoa onyo kwa wanunuzi wa korosho wanaonunua kwa wakulima kwa njia isiyo halali almaarufu kwa jina la ‘Kangomba’ hali inayoweza kusababisha wakulima kushindwa kuendelea na kulima zao hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya maafisa ushirika mkoabi Mtwara yanayojumuisha mikoa mitano, Waziri Mkenda amesema ni muhimu kukemea suala hilo la wanunuzi ili kumsaidia mkulima.
Aidha serikali ina mikakati ya kuwezesha wakulima ili waendelee kulima zao hilo ambapo wanatoa pembejeo na kuwawezesha kwa namna mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirika na kuwawezesha maafisa ushirika na ugani, kwa kufanya hivyo kutasaidia zao hilo kuendelea kufanya vizuri.
Hata hivyo Waziri Mkenda amewashauri maafisa hao kuanzisha mkakati utakaowasaidia wakulima kuwaelimisha kuachana na kangomba lakini pia kuangalia namna ya kufungua SACCOS itakayowasaidia wakulima kuachana na kongamba.
Nae Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege, amesema kuwa mafunzo hayo yanajumuisha vyama zaidi ya 9000
nchini ambapo zaidi ya maofisa 400 watajengewa uwezo.