Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa wito kwa wafanyabiashara kutumia huduma ya msaada wa kitaalamu kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi ili kuepukana na usumbufu wa bidhaa kurudishwa nchini kutokukidhi matakwa ya viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Uthibiti Ubora TBS Hassan A. Juma amesema kuwa huduma hiyo inatolewa shirika la viwango Tanzania TBS ili kusaidia wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango vya nchi husika.

Hassan amesema kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki bidhaa ambayo imethibitishwa na TBS huwa haina kipingamizi lakini zinazokwenda nje huwa wanatoa huduma za ukaguzi kabla ya kwenda nje sambamba na utoaji wa cheti.

‘Kwa bidhaa zinazokwenda nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki huwa tunawapa taarifa ya nini kinahitajika kwa nchi husika kwa upande wa viwango kama mfanyabiashara atakua hana taarifa hizo vilevile huwa tunakaguana kuipima ubora wake kabla ya kuisafirisha na kutoa cheti.’amesema Hassan

Rais Samia:Urithi wa Miradi ya awamu ya 5 unaenda Salama
'Only one King' ya Kiba yazidisha 'streams' milioni 150