Meneja wa mwanamuziki Ali Kiba, Aidan Charlie ameweka wazi kuwa Album ya msanii wake imefanikiwa kufikisha zaidi ya streams Milioni 150 kwenye platforms mbali mbali.

Kiwango cha mauzo ya album hiyo kimewekwa wazi na Meneja wa Ali Kiba, alipokuwa akimjibu shabiki aliyehoji kupitia sehemu ya comment kuwa ni zipi sababu za album hiyo kutofanya vizuri sokoni hasa kupitia

“Ikiwa album ya Ali Kiba ni bora ni kwanini haiuzi sokoni?” Alihoji shabiki.

Muda mfupi baadaye alipokea majibu kutoka kwa meneja Aidan akimfafanulia namna album hiyo ilivyofanya vizuri ndani ya kipindi cha miezi sita pekee tangu ilipotoka rasmi octoba 7 mwaka jana.

“Kuanzia Oktoba 7 hadi sasa hivi ‘Only One King’ ina streams zaidi ya Million 150+ kwenye digital platforms zote, ” amesema Aidan.

‘Only one King’ ya Ali Kiba iliachiwa rasmi mnamo Octoba 7 mwaka 2022 ikiwa na jumla ya nyimbo kumi na sita.

Wasafirishaji bidhaa nje wahimizwa kupima bidhaa zao
Urusi yamshambulia Biden kwa kumfananisha Putin na Joseph Kony wa Uganda