Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa wasani kuanza kulipwa kuanzia mwezi Disemba mwaka huu mara baada ya redio, TV na mitandao ya kijamii kupiga nyimbo zao.
Amesema hayo wakati akizungumza na vijana Jijini Mwanza ambapo amesema Serikali imeimarisha usimamizi wa hakimiliki za wasanii na wataanza kulipwa mirahaba yao kutokana kazi zao kutumiwa.
“Sanaa na utamaduni, sekta hii imekuwa ikikua kwa kasi, miongoni mwa hatua tulizochukua ni kuimarisha usimamizi wa haki miliki za wasanii, nataka kuarifu vijana kuwa kuanzia Disemba mwaka huu wasanii wataanza kulipwa mirabaha yao kutokana na kazi zinazotumiwa kwenye Runinga, Redio na Mitandaoni.” – Rais Samia kwenye mkutano wa vijana Mkoani Mwanza.
Rais Samia amehitimisha ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Mwanza kwa kuhutubia vijana wa Mwanza na kuzindua meli mbili na cherezo.