Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto aitwaye Daines Kefas Mwansasu (06) mwanafunzi wa shule ya Awali- Mlimani
Jeshi hilo limewataja wanaotuhumiwa kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto huyo kuwa ni Judith Amoni Mwansansu (39) Mkazi wa Mwanjelwa na Aive Alex Swalo (17) Mkazi wa Mwanjelwa Mtaa wa Soko jijini humo.
Aidha, Kamanda wa Polisi jijini Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema kuwa tukio hilo lilifanyika Jumanne majira ya saa tatu usiku ambapo jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema, ya kwamba mtoto huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali kwa moto.
“Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mhanga alikuwa ameenda kucheza na rafiki zake na aliporudi nyumbani majira ya jioni ndipo shangazi yake alimuadhibu kwa kumchapa na waya wa umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha na maumivu makali mwilini. Inadaiwa kuwa tarehe 01.08.2018 majira ya asubuhi, watuhumiwa waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto huyo kwa kumuunguza kwa moto sehemu za miguuni na kwenye makalio,” amesema Kamanda Matei.
-
Waziri Mhagama atangaza sheria mifuko hifadhi jamii kuanza kutumika
-
LIVE: Mawaziri 11, Makatibu wakuu 14 wakijadili mradi wa umeme wa maji Rufiji
-
Video: Waziri Mhagama atangaza rasmi kuanza utekelezaji wa sheria mpya PSSSF
Hata hivyo, ameongeza kuwa Mtoto amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kufanyiwa vitendo vya ukatili na shangazi yake akishirikiana na mtoto wake.