Jeshi la Polisi, linawashikilia watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wamekuwa wakitumia silaha kuwaua madereva mbalimbali na kisha kuuza vyombo vyao vya moto yao katika mjiji la Benini uliopo Jimbo la Edo nchini Nigeria.
Mbele ya gwaride la utambuzi Makao Makuu ya Polisi, mmoja wa majambazi hao Williams Abiodun alisema yeye na wenzie wanne kwa kawaida hujigeuza kuwa wahudumu wa eneo hilo ili kuwarubuni madereva wasiokuwa na hatia na kuwapeleka mahali walipowaibia magari yao.
Alisema, “Tunapofika eneo hilo, tunachukua magari yao, tunawaua na kuyauza. tulimuua mtu wa kwanza tukachukua gari lake na kuliuza kwa kampuni ya Kichina. Mtu wa pili alikuwa mwendesha Kekee (Bajaji) ambaye tulimuua na kuuza Kekee yake lakini tulikamatwa tukijaribu kuuza Toyota Sienna ambayo tuliipata wakati wa operesheni ya tatu.”
Akihojiwa mtuhumiwa wa pili alisema, “Abiodun aliniambia kuwa kazi yangu ilikuwa ni kuangalia ni nani anayekuja. Ya kwanza tuliyofanya, alinipa Naira 35,000; Nilipata Naira 55,000 katika operesheni ya pili na tulikamatwa tukijaribu kuuza gari la tatu na jumla tuliwaua watu watatu.”
Kamishna wa Polisi wa Jimbo hilo, Mohammed Dankwara, wakati wa gwaride hilo, alisema washukiwa 135 wa uhalifu wamekamatwa tangu ashike madaraka katika jimbo hilo, na kuongeza kuwa polisi pia walipata Naira milioni 1.2 silaha za kisasa na risasi.