Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, ACP Isack Mushi amesema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa matukio mawili ya vifo vya watoto wawili wanaodaiwa kujinyonga ambapo mmoja alichukua hatua hiyo baada ya kuzuiwa na kaka yake kwenda kuangalia video usiku kwenye mabanda.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kilomba iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amekutwa amefariki baada ya kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia mtandio wake.

Tukio hilo lilitokea Februari 26, 2023 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Muungano Kata ya Kiromba mkoani humo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara ACP Isack Mushi

Uchunguzi wa daktari umebaini chanzo cha kifo ni kukosa hewa baada ya kubanwa na mtandio shingoni ambapo uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Kamanda Mushi amesema tukio la pili, ni la mtoto mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Kijiji cha Mnima amekutwa porini akiwa amenyongwa.

mesema siku ya tukio mtoto huyo alitoka nyumbani na haikujuliakana anakwenda wapi, lakini baadaye mwili wake ulikutwa ukiwa porini ukiwa unaning’inia kwenye mti porini.

Amesema uchunguzi umebaini kuwa marehemu alikuwa anadaiwa Sh8, 000, japo tayari mama yake alikuwa amelipa deni hilo.

'Kigogo' ashtakiwa kwa mauaji, treni iliyoua 43 Ugiriki
Zoran Maki afunguka kilichomuondoa Simba SC