Wachezaji Shomari Kapombe, na Jimmyson Mwanuke wataendelea kukosekena kwenye kikosi cha Simba SC, kufuatia majereha yanayowakabili katika kipindi hiki, huku mwenzao Peter Banda akirudi kikosini.
Wachezaji hao waliachwa Dar es salaam wakati Simba SC ilipokwenda Angola kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ta Primero de Agosto, uliopigwa Jumapili (Oktoba 09), huku Mnyama akiibuka na ushindi wa 3-1 ugenini.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amethibitisha taarifa za kukosekana kwa wachezaji hao watatu kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili, alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatano (Oktoba 12) mchana.
“Tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe ambaye sasa anaendelea kufanya mazoezi akiwa hospitali, ataukosa mchezo wa jumapili lakini michezo itakayofata atakuwepo. Jimmyson Mwinuke pia tutamkosa, taarifa njema ni Peter Banda amerejea kikosini.”
“Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi kurejea kutokea Angola. Kilianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wetu wa Mo Simba Arena na leo kitaingia kambini.”
Katika hatau nyingine Ahmed Ally amesema bado Simba SC haijafuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika licha ya kuongoza kwa mabao 3-1 dhidi ya Primero de Agosto ya Angola.
“Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
Msimu uliopita Simba SC ilipoteza nafasi ya kucheza Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa kwa kupoteza nyumbani 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, ambayo ilikubaki kufungwa mjini Gaberone kwa mabao 2-0.
Mchezo wa Jumapili (Oktoba 16) dhidi ya Primero de Agosto Simba SC itahitaji ushindi ama sare yoyote katika ili kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kucheza Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.