Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa amelitaka Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ kuvisaidia vilabu vinavyoshiriki Michuano ya Kimataifa ili vifanye vizuri na kuwafurahisha watanzania.

Waziri Mchengerwa alitoa agizo hilo wakati akikabidhi zawadi kwa timu ya Taifa ya Soka ya Watu wenye Ulemavu (Tembo Warriors)iliyoshiriki Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Uturuki.

Waziri Mchengerwa amesema: “Ninawaagiza (TFF) kuvisaidia vilabu kuvuka kwenye hatua hii, mvisaidie vilabu vyote sio klabu moja pekee kwa sababu kufanikiwa kwa vilabu hivi ni mafanikio kwa Nchi”

“Niwapongeze Simba kwa kuanza vizuri ila niwaagize Young Africans na uzuri Rais wenu yupo hapa, Muende mkashinde Sudan ili mfuzu hatua ya makundi”

“Mimi naamini mna kikosi kizuri kuliko wao NI LAZIMA MKASHINDE, Wachezaji wajitume dakika zote 90′ wakimbie kwa nguvu na kucheza vizuri. Kufuzu inawezekana”

“Ni viagize vilabu vyote vinavyoshiriki kwenye mashindano ya kimataifa (CAF), Watanzania wanataka ushindi”

Nishati safi ya kupikia kuokoa maisha ya Watanzania
Shirikisho la Soka Afrika laionya Al Hilal