Viongozi wa kundi la mataifa saba yaliondelea kiuchumi duniani G7, wamejadili juu ya kuendelea kuiunga mkono Ukraine kwa kuipatia misaada mbalimbali katika wakati huu ambapo taifa hilo linaendelea kukabiliana na mashambulizi ya Urusi katika miji yake kadhaa ikiwemo mji mkuu Kyiv.

Kansela wa Ujerumani Olaf Sholz amesema, walikubaliana kuwepo kwa vikwazo kadhaa kwa Urusi ambavyo wanaamini vitazidi kuiwekea mbinyo urusi na uchumi wake kwa ujumla ambapo suala la misaada waliokubaliana viongozi hao ni pamoja na ile ya kiutu, kidiplomasia na kisheria pamoja na kulisimamia taifa hilo.

Kutoka kushoto ni Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida na Tume ya Umoja wa Ulaya. Katika picha ya pamoja kwenye mkutano wa G7 huko Schloss Elmau karibu na Garmisch-Partenkirchen, Ujerumani, Juni 26, 2022. Picha na Stefan Rousseau.

Kwa upande wake, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa mwito mataifa hayo ya G7 kuendelea kuiunga mkono nchi yake kwa kuiwekea vikwazo zaidi nishati ya mafuta na gesi kutoka Urusi.

Amesema kikomo cha bei kwa bidhaa hiyo kinapaswa kuwekwa kwa mafuta na gesi kutoka kwa taifa hilo alilolitaja la kigaidi kwenye matokeo ya kuambulia patupu kwenye faida.

Wawili Simba SC kuikosa Primero de Agosto
Ujerumani yaungana na Mataifa ya Afrika UN