Ujerumani imerejea tena katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, baada ya kuchaguliwa katika Baraza hilo sambamba na Nchi nne za bara la Afrika za Sudan, Algeria, Moroco na Afrika ya Kusini.

Kura ya siri, ilipigwa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye nchi wanachama 193, kujaza nafasi 14 kwenye Baraza la Haki za Binadamu lenye viti 47 na Ujerumani imepita kwa kupata kura 167 katika ya 176 zinazowezekana, na sasa itakaa katika baraza hilo kwa miaka mitatu, kuanzia 2023 hadi 2025.

Nchi nyingine zilizofanikiwa kuchaguliwa katika baraza hilo ni Algeria, Bangladesh, Ubelgiji, Chile, Costa Rica na Georgia. Nyingine ni  Kyrgyzstan, Maldives, Moroko, Romania, Afrika Kusini, Sudan na Vietnam, ingawa Venezuela, Korea Kusini na Afghanistan pia zilijaribu lakini zilishindwa kupata kura za kutosha kuziunga mkono.

Hata hivyo, Makundi ya kutetea haki za binadamu yanaukosoa mtindo huo, kwa hoja kwamba unazinyima nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa chaguo huru la nchi zifaazo, na kuzihakikishia nafasi baadhi ya nchi zenye rekodi mbaya ya haki za binadamu.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Louis Charbonneau amekaribisha kushindwa kwa Venezuela, akisema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walipata ushahidi kuwa rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro na maafisa wengine wa serikali yake, wanawajibika katika uhalifu dhidi ya ubinadamu waliotendewa raia wa Venezuela.

Aidha, Wachambuzi wa mambo wanasema uchaguzi huu wa jana ni muhimu kwa sababu utabadilisha mzani wa maoni katika baraza la haki za binadamu lenye migawanyiko na matokeo ya kura katika baraza hilo lenye makao yake mjini Geneva ambapo upande unaoongozwa na nchi za magharibi ulishindwa kwa kura mbili ili kuitisha mdahalo juu ya tuhuma dhidi ya China za uvunjifu wa haki za binadamu katika jimbo la Xinjiang.

G7 yasuka mipango kuiunga mkono Ukraine
Nishati safi ya kupikia kuokoa maisha ya Watanzania