Watu wawili ambao ni wanandoa wamefariki dunia Wilayani Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto Piyaya Kata ya Piyaya wilayani humo.

Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Yusuph Ilembo na kusema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.

Aidha, Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.

Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Ngorongoro, Bilango Ole Senge amesema alikuta miili hiyo ya wanandoa ikiwa kwenye mto huo, pindi alipokuwa anatoka tarafa ya Ngorongoro.

Amesema baada ya kuona hali hiyo alitoa taarifa polisi, Wilaya ya Ngorongoro ambapo polisi iliichukua kwa kuifanyia uchunguzi.

Rapa Rick Ross Kutumbuiza Nchini Kenya
Prof. Tibaijuka awachana viongozi wa serikali ya awamu ya tano