Jijini Arusha watu wasiojulikana wameibuka na kufanya matukio ya uhalifu na utekaji ambapo watoto wadogo watano wametekwa akiwemo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Lucky Vincent, Maureen David.
Ambapo wahalifu hao waliwataka wazazi wa watoto matekwa kupeleka kiasi cha fedha cha shilingi mil.4.5 ili wawaachie watoto wao, na kutishia kurudisha vichwa vya watoto endapo wazazi watashindwa kutimiza masharti yao.
Matukio hayo yametokea katika mtaa wa Olkereyani kata ya Olasiti, ambapo mwenyekiti wao, Daud Safari amesema watoto wengine waliotekwa ni pamoja na Ikram Salim (3), Ayub Fred (3), na Bakari Selemani (3)
Daud Safari ameeleza mbele ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kuwa tukio la kwanza limetokea Agosti 21, ambapo mtoto Moureen David mwenye umri wa miaka 6 alitekwa, na tukio la pili limetokea Agosti 25, mwaka huu ambapo mtoto Ikram ametekwa mida ya saa 12 jioni na watekaji hao kuanza kuwasiliana na babu wa mtoto huyo aliyetambuliwa kwa jina la Kassim Hassan.
”Walimteka jumamosi tukatoa taarifa polisi, Pia waliacha ujumbe wakisisitiza wako na mtoto na kumtaka babu na wazazi wasitoe taarifa polisi wala mahali popote, pia walitaka mawasiliano yote yafanyike kwa ujumbe mfupi wa maneno” ameeleza Safari Daud.
-
Video: Hospitalitali za serikali zitakuwa bora kuliko za binafsi- Makonda
-
Kamanda Mambosasa: Kila mtu ni mtekwaji mtarajiwa
Kutokana na matukio hayo wazazi wamejawa na hofu kubwa iliyowapelekea kuchukua uamuzi wa kuwapeleka watoto shule na kuwarudisha
Aidha Safari amesema ” Awali tulidhani kuna suala la visasi kwa sababu watekaji hao walikuwa wakiandika ujumbe kwenye karatasi na kuupeleka nyumbani kwa wazazi wa watoto, wakisema kama wazazi hao wakitekeleza masharti yao , watawasamehe makosa yote waliyowahi kuwatendea. Lakini tulipowauliza wazazi walisema hawana kumbukumbu kama wamewahi kumkosea mtu”.
Mbunge Lema alilaani matukio hayo na kusema jeshi laPolisi linapaswa kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kukabiliana na mtandao huo wa wahalifu.