Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kumtafuta na kumkamata mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, kwa kueneza uvumi kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

Amesema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na lishe pamoja na shughuli za Maendeleo ya Jamii katika Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara.

Katika hatua nyingine Waziri Gwajima, amepiga marufuku watu wanaoeneza uvumi juu ya chanjo ya Corona ambapo amesema yeye ndio mwenye mamlaka ya kutangaza jambo juu ya afya.

Nchi za SADC ziwainue wanawake - Rais Samia
Elimu bure kupandisha kiwango cha Udahili