Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika ya Kusini , Malusi Gigaba ameomba radhi mara baada ya video yake ya ngono kuvuja mtandaoni.

Waziri Gigaba amesema kuwa video hiyo ilirekodiwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya yeye na mke wake ambapo video hizo zilivuja mara baada ya simu yake kudukuliwa na wahalifu wa mtandaoni mwaka jana.

Amesema video hiyo ilianza kusambaa mara baada ya wahalifu hao wa mtandaoni kumtaka atoe kiasi cha fedha alipochaguliwa kuwa Waziri wa fedha mwaka 2017.

Tayari taarifa juu ya wahalifu hawa zipo mikononi mwa sheria, hivyo uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika.

Gigaba ameomba radhi kwa umma pamoja na familia yake hasa watoto wake, mama yake na mama mkwe wake kwa machungu na aibu kali aliyoisababisha kutokana na kusambaa kwa video yake akiwa faragha.

Rebeca Gyumi aibuka kidedea tuzo ya haki za binadamu za UN
Ndege nyingine aina ya Boeing 737 yaanguka Indonesia