Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewasili Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi kuungana na Timu ya Wataalam wa Afya kufuatilia Ugonjwa Usiojulikana ambao umeripotiwa kutokea hivi karibuni katika Mkoa wa Lindi.

Julai 13, 2022 Wizara ya Afya nchini ilitoa taarifa kuhusu ugonjwa wa ajabu uliokumba mkoa huo ambapo ilisema hadi kufikia Julai 12, 2022 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 13, ambapo watatu kati yao walifariki.

Taarifa ya Wizara hiyo Julai 7, 2022 pia ilipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ruangwa kuwa kumekuwepo na ugonjwa usio wa kawaida kutoka kwenye kituo cha afya cha Mbekenyera.

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ruangwa, Mkoani Lindi.

Taarifa hizo zilidai kuwa ndani ya siku tatu walipokea wagonjwa wawili katika kituo hicho wakiwa na dalili za homa, kuvuja damu puani, maumivu ya kichwa na mwili kuchoka.

Kufuatia hatua hiyo, Wizara ya Afya iliunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na Majanga, Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Utafiti (NIMR), Chuo kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwasili Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Rais 'amkataa' mkandarasi uwezo mdogo
Waangalizi uchaguzi 'wamulika' kampeni Kenya