Waziri wa Maji, Juma Aweso ameonesha kutoridhishwa na kazi iliyofanyika, matumizi ya fedha sambamba na kucheleweshwa kwa mradi wa maji katika wilaya ya Kasulu Jimbo la Kasulu mjini, Mkoani Kigoma katika eneo la Mradi uliopo kata ya Kumunyika.

Akizungumza katika eneo la mradi, Waziri Aweso amemtaka wahandisi wa maji kuhakikisha wanatekeleza miradi kwa ufanisi na kwa wakati wakizingatia matumizi sahihi ya fedha.

Amesema ni muhimu kazi hiyo ikafanyika ndani ya miezi mitatu wananchi wapate maji kwa mikakati ya muda mfupi wakati Utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji Miji 28 Kasulu ukiendelea.

Waziri Aweso pia ametaka kukaa pembeni kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Kasulu Mjini Eng. Riziki Nyamtega na kuahidi kuleta uongozi mpya Wilayani hapo na kuisuka Mamlaka hiyo ya Maji.

Hata hivyo, amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Nzega, Eng. Athumani kilundumya kuisimamia Mamlaka hiyo katika kipindi cha Utekelezaji wa maagizo yake akiendelea kuiunda Mamlaka.

Rais Samia aagiza mageuzi haki jinai
Ruto amshushia lawama Kenyatta