Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo , kuongea na wananchi pamoja na watumishi wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na RC Sendiga amesema Majaliwa atawasili mkoani Rukwa tarehe 14 Desemba,2022 na atahitimisha ziara yake tarehe 16 Desemba 2022 ambapo atetembelea Wilaya tatu za Nkasi,Kalambo na Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga

RC Sendiga amebainisha kuwa kazi zitakazofanyika ni Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Sekondari Paramawe – Nkasi na kutembelea mradi wa jengo la upasuaji na jengo la huduma za dharura (EMD), Hospitali ya Wilaya Nkasi.

Majaliwa pia anatarajiwa kuweka jiwe la msingi jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Matai-Kasesya na Kukagua ujenzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga huku Mkuu huyo wa Mkoa akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo yatakayotembelewa.

Shambulizi Hotelini lachukua uhai wa watatu
Rais Ruto 'amkubali' mpinzani wake