Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo jumatano tarehe 17 Mei 2023.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye ukumbi wa Anatouglou unaratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Kwa sasa Serikali imeendelea kuwasihi wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.