Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia, Harry Kalaba, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, akidai kuwa Rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu ameshindwa kupambana na rushwa.
Kalaba amesema uamuzi wake umetokana na kiwango cha juu cha rushwa ambayo inafanywa na watu ambao wanatarajiwa kuwa suluhisho
Amesema tayari amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Lungu, na kwamba amechukua uamuzi huo kwa moyo mzito, hata hivyo Msemaji wa Rais, Amos Chanda, amesema Ikulu bado haijapokea barua ya kujiuzulu kwa Kalaba.
-
Mwanachama wa NCCR- Mageuzi ajivua uanachama
Kalaba anakuwa Waziri wa tatu kuondoka ndani ya serikali ya Rais Lungu baada ya kutimuliwa kwa Mawaziri wawili akiwemo Waziri wa Mipango na Waziri wa Habari na Utangazaji.
Kalaba, ambaye ni Mbunge wa chama tawala cha Patriotic Front (PF), anatajwa kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka 2021 ikiwa Lungu atajiweka pembeni.