Rais John Pombe Magufuli ameleta habari njema kwa wote wanaoidai Serikali na kusema kuwa atatoa kiasi cha fedha Bilioni 200 za Kitanzania kwa lengo la kulipa madeni ya ndani ya nchi ambayo serikali inadaiwa.

Magufuli amesema zoezi hilo litaanza rasmi mapema februari mwaka huu ikiwa ni hatua mojawapo ya kusaidia nchi kuinuka kiuchumi kwa kupunguza madeni na kufanya maendeleo mengine.

“Nimepanga kuanzia mwezi ujao madeni yote ya ndani ya wanaoidai serikali yatakapokuwa yamehakikiwa, nitatoa Tshs Bilioni 200 ili yakalipwe’’ amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo ameongezea kuwa angeweza kuyalipa madeni hayo hata kesho ila kwanza anapisha kamati ya uhakiki kufanya kazi yao ya kuhakiki madeni yote ili kujiridhisha kisha malipo yatafanyika mapema mara baada ya uhakiki huo kukamilika.

‘’Uhakiki ukifanywa mapema, madeni yataanza kulipwa mapema, na kuwasaidia watu hawa kuendelea kufanya biashara zao.” Rais Magufuli amemaiza kwa kusema hivyo.

Ameyasema hayo leo January 3, 2017 akiwa Ikulu pindi alipokuwa akimuaga Gavana wa Benki Kuu (BoT) ambaye amemaliza muda wake, Profesa Benno Ndulu aliyeongozana na Gavana mpya wa (BoT) Frolens Luoga Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya nje ajiuzulu
Kisa cha walimu tisa kufukuzwa kazi