Katika kuadhimisha siku ya kupinga kujiua duniani mwanasaikolojia tiba, Isaac Lema, ameeleza hali ya matukio ya kujiua, sababu na namna yanavyoweza kuzuilika.
Katika kuadhimisha siku ya kupinga kujiua duniani mwanasaikolojia tiba, Isaac Lema, ameeleza hali ya matukio ya kujiua, sababu na namna yanavyoweza kuzuilika.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha watu 800,000 hujiua kwa mwaka duniani kote, huku kwa takwimu za Tanzania kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 zinaonyesha watu watano hadi tisa hujiua kati ya watu 100,000.
Lema amesema zipo sababu nyingi zinazopelekea watu kujiua, ugonjwa wa sonona (Depresion)ukiongoza.
Aidha ameeleza kuwa yapo magonjwa mengine ya akili yanayopelekea mtu kusitisha uhai wake.
”Visa vinavyo changia mtu kusitisha uhai wake sio tu wivu wa mapenzi, ni mpaka awe na vihatarishi vinanavyoungana kupeleka kujiua hakuna sababu moja, lakini matukio hasi mara nyingi huchangia hali ya kufikia kupata maradhi ya ugonjwa wa akili,” amesema Msaikolojia Lema.
”Ambaye wazo la kutaka kujiua huwa linajirudia mara kwa mara na wakati mwingine linamsumbua mtu kiasi kwamba anashindwa kufanya mambo yake ya kawaida, huwa tunashauri ikifikia hali hiyo amshirikisha mtu wa karibu, inasaidia kupunguza ile hali ya kiisia kama haitasaidia basi ni vizuri akaonana na wataalamu,” ameongeza Lema.