Nyota wa muziki toka Nigeria Tiwatope Savage, maarufu Tiwa Savage (40) amesema kuwa aliwahi kukata tamaa na kutaka kuacha muziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jarida la NewYorkTimes, nyota huyo wa Nigeria amesema kuwa mwaka 2010 alikuwa karibu kuacha muziki baada ya kutoa wimbo wake “Love Me, Love Me, Love Me.”

Wimbo huo ulifungiwa na shirika la habari Nigeria (NAN) kitu kilichopelekea hata baadhi ya matamasha yake kuahirishwa na kufanya msanii huyo akate tamaa kabisa na masuala ya muziki.

Akielezea sababu iliyomsukuma kurudi kwenye biashara ya muziki Tiwa Savage amesema, “Baada ya kufanya maamuzi ya kuacha, kulikuwa na wasichana wengi waliokuwa wakinitumia ujumbe mara nimependa hereni zako, au mara nimependa ‘tattoo’ yako na hapo ndipo niliposema acha nirudi kwa ajili ya wasichana hawa.”

“Mpaka sasa ninawahamasisha wasichana wengi lakini wao ndio walionihamasisha kurudi kwenye muziki,” ameongeza Tiwas Savage.

Wazo la kujiua ni dalili za ugonjwa wa akili
"Jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu ni letu sote" - CGI Makakala

Comments

comments