Mkongwe wa muziki wa bongofleva Bwana Misosi amesema amesaidia baadhi ya wasanii akiwemo Man X pamoja na msanii kutoka Konde gang Harmonize kwenye kazi zao za sanaa bila hata kuwadai pesa kwa sababu hawana uwezo wa kumlipa.

Kwa mujibu wa East africa Radio Misosi amesema beat la wimbo wake wa nitoke vipi limetumiwa na Man X, pia beat lake la mabinti wa kitanga ametumia Harmonize kwenye wimbo wake wa ‘never give up’.

“Kuna wasanii wametumia mgongo wangu kwenye kazi zao kama Man X ametumia beat la wimbo wangu wa nitoke vipi, pia wimbo wa ‘Never Give Up’ ya Harmonize ni beat langu kwenye wimbo wa mabinti wa kitanga, Harmonize alitaka kunilipa nikamwambia gharama zake hataziweza” amesema Bwana Misosi.

Bwana Misosi amesema nyimbo zake za nitoke vipi na mabinti wa kitanga zilimpa mafanikio makubwa na kumfanya kufahamika ndani na nje ya Tanzania.

Rais aliyeng'olewa madarakani alazwa hospitali - Mali
Manara: Hizo ni propaganda za kuvuruga utulivu Simba SC