Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa Watanzania kuhifadhi na kuuutunza Mlima Kilimanjaro, ili uendelee kuinufaisha nchi.
Waziri Jafo, metoa wito huo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malecela aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kukabiliana na matukio ya uchomaji moto Mlima Kiliamanjro.
Amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha matukio hayo yanakoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo
Aidhsa ameongeza kuwa, pamoja na Serikali kuunda timu ya kufanya utafiti wa matukio ya moto wananchi wana wajibu wa kuacha vitendo vya ukataji miti na uchomaji moto eneo la hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis alisema Serikali kupitia Taasisi mbalimbali za ndani ya nchi zikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine, na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela vinaendelea kufanya tafiti kuhusu suala hili.