Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Wizara ya Nishati ina wajibu wa kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya nishati mbadala kwa lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Majaliwa ameyasema hayo jijini Dodoma, baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya Nishati inayofanyika katika viwanja vya Bunge.
Amesema, “Serikali kupitia Wizara ya Nishati pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) imeunda kamati ya kitaifa inayoratibu utoaji elimu na kuonesha fursa za wajasiriamali ambao watahitaji kuingia kwenye sekta hii ya matumizi ya nishati mbadala.”
“Anzeni na taasisi za elimu majeshi, kambi za wakimbizi na kila mahali penye watu zaidi ya mia moja nataka maeneo hayo yawe anzilishi na tuachane na kukata miti. Tunataka watanzania waanze kutumia nishati mbadala, huu ndio muelekeo wa Taifa letu,” ameeelekeza Majaliwa.