Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar hapo jana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa jana katika uwanja wa Kaitaba.
Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kupata ushindi uliozidi goli moja kwenye ligi na ushindi dhidi ya Kagera umeipa Yanga pointi tatu na hatimaye wamefikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi zao sita za ligi.
Yanga inapanda kwenye msimamo kutoka nafasi ya sita hadi ya kwanza ikiwa sawa kwa pointi na Azam ambayo ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 Mwadui huku Yanga na Azam zote zikisubiri matokeo ya mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa.
-
Kamusoko kukaa nje ya dimba kwa wiki mbili
-
Kwa Man City hii tutegemee makubwa msimu huu
-
Crystal Palace wapata ushindi wa kwanza EPL, wampiga bingwa mtetezi
Simba wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 11, pointi moja nyuma ya Yanga na Azam na endapo wakishinda dhidi ya Mtibwa leo watafikisha pointi 14 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza.
Mtibwa pia ina nafasi nzuri ya kuongoza ligi endapo itashinda mchezo wa leodhidi ya Simba, Mtibwa ina pointi 11 sawa na Simba na Singida United (tayari Singida imecheza mechi sita) Mtibwa nayo ikipata sare itafikisha pointi 12 sawa na Yanga na Azam.