Klabu ya Manchester City iko katika ubora wa hali ya juu hivi sasa katika ligi kuu ya Uingereza, klabu hiyo inayofundishwa na kocha Pep Guadiola hapo jana imepata ushidi mnono wa mabo 7-2 dhidi ya Stoke City katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Etihad Stadium.

Mabao ya Man City katika mchezo wa jana yalifungwa na Gabiel Jesus aliyefunga mabao 2, Raheem Sterling, Bernardo Silva, David Silva, Leroya Sane na Fernandinho wakati mabao ya Stoke yakifungwa na Mame Biram Diouf pamoja na bao la kujifunga la Kyle Walker.

Ikiwa tayari imecheza michezo 8 tu ya ligi kuu klabu hiyo imefunga jumla ya mabao 29 na kufungwa mabao 4 tu huku ikiwa kileleni mwa msimamo wa EPL kwa pointi 22 ikifuatiwa na Man Utd yenye pointi 20.

Bado ni mapema sana kusema Man City watatwaa ubingwa lakini kwa ubora unaoonyeshwa na kikosi cha Pep Guardiola ni wazi kwamba msimuu huu City watatoa upinzani mkubwa katika kinyang’anyiro cha ubigwa wa EPL, kama sio kuchukua kombe hilo kwani wanacheza kwa ubora wa hali ya juu sana.

Msimu uliopita Man City ilimaliza katika nafasi ya tatu ikiwa imefunga mabao 80 na kufungwa mabao 39 ikikusanya jumla ya pointi 78 ikiwa nyuma ya mabingwa Chelsea kwa pointi 15.

Ukiwa ni msimu wake wa Pep Guardiola ambaye hakushinda kikombe chochote msimu uliopita kwa sasa anaonekana kuhimarisha kikosi chake hasa katika safu ya ushambuliaji akiwatumia Gabriel Jesus, Raheem Sterling, Leroya Sane na Sergio Aguero.

Kiungo wa Hispania David Silva ndiye anaongoza kwa kutoa pasi za magoli (Assists) 6 huku washambuliaji Raheem Sterling, Gabriel Jesus na Sergio Aguero wakiwa wamefunga mabao 18 kwa pamoja mpaka sasa.

Kigwangalla anena kuhusu vurugu za uchaguzi Kenya
Vidio: Sababu za JPM kutokuongeza mishahara kwa watumishi wa Umma