Yanga imeondolewa rasmi katika ligi ya mabingwa Afrika kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Zesco United ya Malawi.
Zesco ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jesser Were mnamo dakika ya 25 kabla ya Yanga kusawazisha kwenye dakika ya 31 kupitia kwa Sadney Urikhob.
Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika Yanga na Zesco walikuwa na matokeo sawa ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 79, Abdulaziz Makame alijifunga na kuwapa Zesco bao la pili alipokuwa kwenye harakati za kuokoa mpira.
Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 ambayo yamewafanya waondolewe kunako Ligi ya Mabingwa sasa watacheza Shirikisho Afrika.
Pia, katika mchezo huo, Lamine alipewa kadi nyekundu mnamo dakika ya 90 kwa kucheza mchezo usio wa kiungwana.