Eliud Wekesa maarufu kama ‘Yesu wa Tongaren’ atabaki kuwa kizuizini kwa siku nne zaidi, ili kutoa nafasi kwa uchunguzi dhidi yake kufuatia madai kutoa mafunzo potovu katika kanisa lake.
Mahakama ya Bungoma imetoa uamuzi uamuzi huo hii leo, Mei 12, 2023 na kusema Polisi walimtaka kiongozi huyo wa dhehebu la New Jerusalem kufika kituoni kwa mahojiano kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka, na Yesu huyo alitii na kufika kwa wakati kama ilivyotakikana na chombo hicho cha usalama.
Wekesa amekuwa akijitangaza kuwa yeye ndiye Yesu ambapo pia ana malaika wake anaosema wanamsaidia katika kazi yake kama kristo mwana wa Mungu na akimiliki malaika wake sambamba na wanafunzi 12 kama ilivyokuwa katika Bibilia na wakati wa Yesu Kristo mwana wa Mungu.