Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Afrucans wataondoka jioni ya kesho kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kesho visiwani humo.

Kikosi cha Young Africans leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam tayari kwa safari ya leo majira ya Alasiri.

Young Africans wataondoka na kikosi wachezaji 26 pamoja na benchi lake zima la ufundi tayari kwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya pemba Saa 2.30 usiku wa kesho.

Kikosi kamili cha Young Africans kinachokwenda Zanzibar ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya na Ali Mustafa ‘Barthez’.

Mabeki ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Vincent Andrew, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Juma Abdul na Oscar Joshua.

Viungo ni Haruna Niyonzima, Justin Zulu, Simoni Msuva, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashuiya, Deus Kaseke, Saidi Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko na Yussuf Mhilu.

Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe, Emmanuel Martin, Obrey Chirwa na Matheo Anthony.

Katika michuano hiyo, Young Africans watamkosa beki wao kutoka nchini Togo, Vincent Bossou aliyekwenda nchini Senegal kujiunga na timu yake ya taifa, kwa maandalizi ya mwisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Januari 14, 2017 nchini Gabon.

Wakati huo huo Simba nao wanatarajia kusafiri kesho kuelekea kisiwani Unguja tayari kwa michuano ya Mapinduzi CUP.

Bondia Francis Cheka afungiwa
Roberto Firmino Kufikishwa Mahakamani