Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kimeanza safari ya kuelekea nchini Mali, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itacheza dhidi ya AS Real Bamako Jumapili (Februari 25), mjini Bamako katika Uwanja wa Machi 26 majira ya saa kumi kwa saa za Mali, sawa na saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mapema leo Alhamis (Februari 23) majira ya Alfjiri kikosi cha 24, Maafisa wa benchi la Ufundi na Baadhi ya Viongozi wa Young Africans walianza safari jijini Dar es salaam, kuelekea Bamako wakipitia Adis Ababa-Ethiopia.

Msafara huo umeondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ambapo utatua Addis Ababa- Ethiopia majira ya saa 4:40 asubuhi Kisha utaondoka kuelekea Mali na kuwasili katika jiji la Bamako majira ya saa 8:40 Mchana.

Orodha ya wachezaji iliyotajwa kwenye msafara huo walinda lango ni ?? Djigui Diarra, Metacha Mnata, na Erick Johora

MABEKI WA PEMBENI NI: Djuma Shabani, Kibwana Shomari, Joyce Lomalisa na David Bryson

MABEKI WA KATI NI: Mamadou Doumbia, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca
VIUNGO WAKABAJI NI: Yannick Bangala, Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Abubakar Sure Boy na Mudathir Yahya

VIUNGO WASHAMBULIAJI NI: Stephane Aziz Ki,Jesus Moloko, Dickson Ambundo, Farid Mussa na Tuisila Kisinda

WASHAMBULIAJI WA KATI ni: Fiston Mayele, Kennedy Musonda, na Clement Mzize

Kabla ya kuanza safari jijini Dar es salaam Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe alizungumza na waandishi wa habari na kuesema maandalizi yao kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa tatu Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Real Bamako yamekamilika na wanatarajia kuwa na mazingira mazuri ya kupambana ugenini.

Kamwe amewahimiza Mashabiki na Wanachama wa Young Africans waliobaki nchini kuendelea kuwa na imani n a timu yao, huku wakiiombea kupata matokeo mazuri ili iweze kujiweka kwenye mwenedelezo wa kupata alama chanya ambazo zitawawezesha kufikia malengo ya kucheza Robo Fainali.

Simba SC kuifuata Vipers SC
Kimbunga Freddy: Wanne wafariki, OCHA watoa tamko