Msafara wa Kikosi Cha Wachezaji 25 wa Klabu ya Simba SC pamoja na Maafisa wa Benchi la ufundi na baadhi ya Viongozi unatarajia kuondoka leo alhamis (Februari 23) majira ya jioni kuelekea Nchini Uganda, kwa ajili ya ya Mchezo wa mzunguuko watatu wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Vipers SC.

Simba SC inaelekea Uganda ikiwa na deni kubwa la kusaka ushindi ili kufufua matumaini ya kuwa sehemu timu ambazo zitaanza kufikiriwa huenda zikacheza Robo Fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu katika ukanga wa Afrika.

Mkakati wa kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Vipers SC, umekuja baada ya miamba hiyo ya Msimbazi kupoteza michezo miwili ya Kundi C, dhidi ya Horoya AC ya Guinea kwa kufungwa 1-0 ugenini mjini Conakry, kisha ikapoteza dhidi ya Raja Casablanca nyumbani Dar es salaam kwa kufungwa 3-0.

Taarifa kutoka Simba SC zinaeleza kuwa, Kabla ya Kikosi cha Klabu hiyo kuondoka Nchini, wachezaji watafanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kwenye Uwanja wa Mo Arena kwa ajili ya kuiweka miili sawa.
Mchezo wa Vipers SC dhidi ya Simba utapigwa Jumamosi ya February 25 kwenye Uwanja wa St Mary’s wenye uwezo wa Kuchukua Mashabiki Elfu 25.

Wanafunzi A-Level kusoma kwa miaka mitano
Young Africans yaifuata AS Real Bamako