Wanafunzi watakaofuzu kujiunga na kidato cha tano (A-Level), sasa watatakiwa kusoma kwa hadi miaka mitano, iwapo serikali itaidhinisha huo mpya wa kidato cha nne na cha sita kuanzia sasa nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya marekebisho katika mtaala wa A-Level, muda wa umiliki wa A-Level utakuwa usiopungua miaka miwili na usiozidi miaka mitano ili kuongeza ushirikishwaji ambapo hapo awali, wamekuwa wakisoma Senior Tano na Sita kwa miaka miwili.

Watahiniwa katika chumba vha mtihani. Picha ya The Independent Uganda.

Karatasi ya Jumla, ambayo hapo awali ilikuwa ikitolewa na wanafunzi wote, itabadilishwa na uwepo wa masomo ya kisasa kama vile ujuzi wa jumla, ICT na utafiti, elimu ya fedha, lishe ya kimsingi, mabadiliko ya hali ya hewa, takwimu za utendaji kazi na kujenga amani.

Aidha, wanafunzi ambao watafeli mitihani ya Uganda ya ‘Advanced Certificate of Education’ – (UACE) sasa watahitajika kurudia somo ambalo hajalifaulu kwani awali, mwanafunzi aliyeshindwa kupata ufaulu wa kanuni mbili, alihitajika kurudia mtihani mzima.

Francis Baraza aipeleka Simba SC Robo Fainali
Simba SC kuifuata Vipers SC