Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo wakati wa hotuba yake kwa nchi za Magharibi kuhusu Ukraine, baada ya kusimamisha mkataba wa kihistoria wa udhibiti wa silaha za nyuklia na kutangaza kuwa mifumo mipya ya kimkakati imewekwa kwenye jukumu la kupambana na kutishia kuanza tena majaribio ya nyuklia.

Takribani mwaka mmoja baada ya kuamuru uvamizi huo ambao umezua makabiliano makubwa zaidi na nchi za Magharibi katika miongo sita, Putin alisema Urusi itafikia malengo yake na kuzishutumu nchi za Magharibi kwa kujaribu kuiangamiza.

Amesema, “Wasomi wa nchi za Magharibi hawafichi madhumuni yao. Lakini pia hawawezi kushindwa kutambua kwamba haiwezekani kuishinda Urusi kwenye uwanja wa vita,” aliwaambia wasomi wa kisiasa na kijeshi wa nchi yake.”

Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Picha ya ABC News.

Putin ameongeza kuwa, Marekani inageuza vita hivyo kuwa mzozo wa kimataifa, Putin alisema Urusi inasitisha ushiriki wake katika Mkataba Mpya wa START, mkataba wake mkuu wa mwisho wa udhibiti wa silaha na Marekani.

Mkataba huo uliosainiwa na Rais wa Marekani wa wakati huo Barack Obama na mwenzake wa Urusi Dmitry Medvedev mwaka 2010, mkataba huo unaweka idadi ya vichwa vya kimkakati vya nyuklia ambavyo nchi hizo zinaweza kupeleka.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinkenke alisema hatua ya Putin ni ya kusikitisha sana na kutowajibika huku Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa inafanywa dunia kuwa sehemu hatari zaidi na kumtaka Putin kufikiria upya.

Makamu wa Rais mgeni rasmi kongamano la uwekezaji
Jean Baleke awatuliza mashabiki Simba SC